Tangazo la Nafasi za Kazi za Mkataba – Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

Mwajiri: Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
Aina ya Ajira: Mkataba wa mwaka mmoja
Nafasi: Msaidizi wa Hesabu (Accounts Assistant) – Nafasi 3
Mahali: Wilaya ya Kishapu
Muda wa Mwisho wa Kutuma Maombi: 15 Mei, 2025 saa 3:30 Asubuhi


🧾 Maelezo ya Nafasi

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu anawatangazia wananchi wote wenye sifa kuomba nafasi tatu (3) za Msaidizi wa Hesabu (Accounts Assistant) kwa mkataba wa mwaka mmoja.


✅ Sifa za Muombaji

  • Awe raia wa Tanzania
  • Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 45
  • Elimu ya kidato cha nne au kuendelea
  • Awe amesoma masomo ya Uhasibu
  • Cheti cha ATEC Level II au “Foundation Level” kutoka NBAA
  • Awe mwaminifu
  • Awe na wadhamini wawili waliothibitishwa kwa barua
  • Uzoefu wa kazi wa mwaka mmoja au zaidi katika fani hiyo
  • Awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote ndani ya Wilaya ya Kishapu
  • Awe na afya njema

🛠️ Majukumu ya Kazi

  • Kuandika na kutunza “Register” za shughuli za uhasibu
  • Kuandaa hati na malipo ya fedha
  • Kutunza majalada na kumbukumbu za uhasibu
  • Kupeleka nyaraka za uhasibu benki
  • Kufanya usuluhisho wa masurufu, fedha, hesabu, na benki kwa ujumla

💰 Mshahara

  • TGS B – Tshs. 450,000/= kwa mwezi

📌 Masharti ya Jumla

  • Kuwa tayari kufanya kazi katika kituo chochote cha afya ndani ya Wilaya ya Kishapu
  • Mkataba wa mwaka mmoja kwa kuzingatia maadili ya kazi
  • Waombaji watakaochaguliwa wataitwa kwenye usaili
  • Maombi yaambatane na nakala za vyeti halisi na maelezo binafsi (CV)
  • CV ijumuishe wadhamini wawili, picha mbili za “passport size”, na nakala za:
    • Cheti cha kuzaliwa
    • Cheti cha NIDA au Passport
    • Vyeti vya elimu

Siku ya usaili, waombaji waje na vyeti halisi vya shule, taaluma, kuzaliwa, na kitambulisho cha taifa.

  • Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria
  • Maombi yaandikwe kwa usahihi na kuambatishwa namba ya simu

📬 Jinsi ya Kutuma Maombi

Tuma barua yako ya maombi iliyosainiwa na viambatanisho vyote muhimu kwa anuani:

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W)
S.L.P. 1288,
22 Barabara ya DED-DC,
37582 KISHAPU

🕓 Mwisho wa kutuma maombi: 15 Mei, 2025 – Saa 3:30 Asubuhi


To apply for this job please visit ajirapoint.com.

Related Jobs