Nafasi za Kazi za Mkataba – Halmashauri ya Wilaya ya Muleba

Mwajiri: Halmashauri ya Wilaya ya Muleba
Aina ya Ajira: Mkataba wa mwaka mmoja
Tarehe ya Tangazo: 07/05/2025
Mwisho wa Kutuma Maombi: 20 Mei 2025, saa 3:30 Asubuhi


πŸ“’ Nafasi Zinazotangazwa

1. Mwandishi wa Habari wa Redio – Nafasi 3

Sifa za Muombaji:

  • Elimu ya kidato cha nne au sita na ufanisi katika Kiswahili, Kiingereza, na Sanaa
  • Cheti cha fani ya Uandishi wa Habari kutoka chuo kinachotambulika na Serikali
  • Mafunzo ya mwaka mmoja kwenye kazi ya Utangazaji/Uandishi wa Habari
  • Mwadilifu, raia wa Tanzania, na mwenye Kitambulisho cha Taifa (NIDA)

Majukumu:

  • Kukusanya habari za matukio mbalimbali
  • Kurekodi taarifa za Redio ndani na nje ya nchi
  • Kufanya kazi chini ya Mwandishi wa Habari mzoefu

Mshahara: TGS B


2. Fundi Mitambo Msaidizi – Nafasi 2

Sifa za Muombaji:

  • Kidato cha nne na kuendelea
  • Masomo ya ufundi, mawasiliano, au kompyuta
  • Uzoefu wa mwaka mmoja kwenye kazi ya mitambo ya redio
  • Ufanisi katika Kiswahili na Kiingereza
  • Asiwe na historia ya makosa ya jinai
  • Raia wa Tanzania na awe na NIDA

Majukumu:

  • Kuendesha na kutunza vifaa vya redio
  • Kutekeleza usafi wa vifaa
  • Kudhibiti na kuratibu huduma za mitambo
  • Kuandaa bajeti ya matengenezo ya vifaa
  • Kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa

Mshahara: TGS B


3. Mzalishaji wa Vipindi / Mtengeneza Maudhui Msaidizi – Nafasi 1

Sifa za Muombaji:

  • Kidato cha nne na kuendelea
  • Mafunzo ya uzalishaji, ufundi, au mawasiliano
  • Uzoefu wa mwaka mmoja katika uzalishaji wa vipindi
  • Ufanisi katika Kiswahili na Kiingereza
  • Asiwe na historia ya makosa ya jinai
  • Raia wa Tanzania na awe na NIDA

Majukumu:

  • Kusaidia kwenye utayarishaji wa vipindi vya redio
  • Kurekodi na kutengeneza muziki na programu za elimu
  • Kuandaa sauti na kufanya uhakiki wa script
  • Kazi nyingine yoyote atakayopangiwa

Mshahara: TGS B


πŸ“Œ Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji

  1. Umri: Miaka 18–45
  2. Asiwe na rekodi ya uhalifu
  3. Aambatishe nakala za vyeti vya elimu na kuzaliwa
  4. Awasilishe CV iliyo kamili yenye wadhamini 3
  5. Alete picha moja ya “passport size”
  6. Matokeo ya “Testimonials”, “Provisional results”, na slips hayatakubaliwa
  7. Vyeti vya nje viambatane na uthibitisho wa NACTE/NACT
  8. Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili
  9. Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria

πŸ“¬ Jinsi ya Kutuma Maombi

Anuani ya Kutuma:

MKURUGENZI MTENDAJI,
HALMASHAURI YA WILAYA,
S.L.P 131, MULEBA
πŸ“§ [email protected]

πŸ•“ Mwisho wa kutuma maombi: 20 Mei 2025 saa 3:30 Asubuhi


To apply for this job email your details to ded@muleba.go.tz

Related Jobs