Tangazo la Nafasi za Kazi – Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge (16 Juni 2025)
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, mkoani Tabora, imetangaza nafasi mpya za ajira kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa Watanzania wenye sifa stahiki. Tangazo hili linazingatia kibali kilichotolewa na Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb. Na. FA.97/288/01/9 ya tarehe 29/04/2025. Nafasi hizi ni kwa kada tatu muhimu zenye jumla ya nafasi 13 za ajira. Zinalenga kuongeza ufanisi katika idara mbalimbali...