Halmashauri ya Mji Masasi imetangaza nafasi mpya za ajira kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kufuatia kibali kutoka kwa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia barua yenye Kumb. Na. FA.97/228/01/A/25 ya tarehe 29 Aprili 2025. Mkurugenzi wa Mji Masasi anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa stahiki kujaza nafasi 14 za ajira katika kada za udereva, uendeshaji wa ofisi, na utunzaji wa kumbukumbu.
Nafasi hizi zinajumuisha majukumu mbalimbali kama vile kuendesha magari ya serikali, kutunza na kusambaza nyaraka, kuchapa nyaraka za kawaida na za siri, na kusimamia mzunguko wa majalada ofisini. Waombaji wanatakiwa kuwa na elimu ya sekondari, vyeti vya taaluma vinavyotambulika na Serikali, pamoja na uzoefu maalum kwa kada husika.
Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo rasmi wa Ajira Portal: https://portal.ajira.go.tz kabla ya 29 Juni 2025. Waombaji wote wanatakiwa kuambatanisha barua ya maombi, vyeti halisi vya taaluma, nakala za vyeti vya kuzaliwa, picha za “passport size” mbili, na CV yenye maelezo ya kina.
📌 Nafasi Zinazotangazwa
- Dereva Daraja la II – Nafasi 5
- Kidato cha Nne, leseni daraja E/C, uzoefu wa mwaka 1 bila ajali, cheti cha Basic Driving kutoka VETA au chuo kinachotambulika.
- Mshahara: TGS B1
- Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 5
- Kidato cha Nne/Sita, Diploma ya Uhazili au NTA Level 6, ujuzi wa hatimkato (maneno 100 kwa dakika), matumizi ya kompyuta (Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher).
- Mshahara: TGS C1
- Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 4
- Kidato cha Nne/Sita, Diploma ya Utunzaji Kumbukumbu (NTA Level 6), ujuzi wa kutumia kompyuta.
- Mshahara: TGS C1