Halmashauri ya Mji Njombe inatangaza nafasi 10 za kazi kwa Watanzania wenye sifa kupitia kibali cha ajira cha tarehe 29/04/2025. Nafasi zinazotangazwa ni kwa ajili ya Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II, Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II, na Dereva Daraja la II. Waombaji wanahitajika kuwa na elimu ya sekondari na stashahada husika, pamoja na ujuzi wa kompyuta kwa kada za uhasibu na utunzaji wa kumbukumbu. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 02/07/2025 kupitia mfumo wa ajira wa Serikali: https://portal.ajira.go.tz
Nafasi Zinazotangazwa:
- Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 2
- Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 4
- Dereva Daraja la II – Nafasi 4
Waombaji wote wanapaswa kuwa raia wa Tanzania, wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45, na kuwasilisha vyeti halali vya taaluma na elimu. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi. Maombi yote yatatumwa kwa njia ya kielektroniki pekee.