Idara: Afya
Muda wa Mkataba: Miezi sita
Mwisho wa Kutuma Maombi: 20 Mei 2025, saa 3:30 Asubuhi
Mahali: Wilaya ya Liwale
๐งโโ๏ธ 1. Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II (ANO)
Idadi ya Nafasi: 15
Majukumu:
- Kutoa huduma za uuguzi
- Kukusanya takwimu muhimu za afya
- Kuelekeza kazi wauguzi walio chini yake
- Kutoa elimu kwa jamii kuhusu matatizo ya kiafya
- Kutoa huduma za uzazi na kinga
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake
Sifa za Muombaji:
- Awe na Stashahada (Diploma) ya Uuguzi kutoka chuo kinachotambulika
- Leseni ya Uuguzi na usajili kutoka Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania
Mshahara:
- Kwa mujibu wa TGHS B
๐ 2. Mtenkolojia Msaidizi โ Dawa
Idadi ya Nafasi: 2
Majukumu:
- Kuandaa mahitaji ya dawa na vifaa tiba
- Kuagiza, kuhifadhi na kugawa dawa na vifaa tiba
- Kuandaa taarifa za matumizi ya dawa
- Kutunza kumbukumbu za dawa na vifaa tiba
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake
Sifa za Muombaji:
- Kidato cha nne na mafunzo ya mwaka mmoja kwenye fani ya afya ya dawa
Mshahara:
- Kwa mujibu wa TGHS A
๐ฉบ 3. Daktari Daraja la II (MO)
Idadi ya Nafasi: 1
Majukumu:
- Kutoa tiba kwa wagonjwa wa kawaida na dharura
- Kusimamia elimu ya afya na huduma za tiba
- Kudhibiti milipuko na kuandaa takwimu za afya
- Kufanya tathmini za huduma za afya
- Kuandaa mipango ya bajeti na huduma
- Kutoa huduma za outreach
- Kufanya kazi nyingine yoyote atakazopangiwa na mkuu wake
Sifa za Muombaji:
- Shahada ya Udaktari kutoka chuo kinachotambulika
- Umehitimu mafunzo ya “Internship” ya mwaka mmoja
- Usajili wa Baraza la Madaktari Tanzania
Mshahara:
- Kwa mujibu wa TGHS E
๐ Masharti kwa Waombaji Wote
- Raia wa Tanzania
- Umri: Miaka 18 hadi 45
- Waambatishe vyeti vya kitaaluma, cheti cha kuzaliwa na CV
- CV ijumuishe majina na namba za simu za wadhamini watatu
- Picha moja ya “passport size” ya hivi karibuni
- “Testimonials”, “Provisional results” na matokeo ya kidato cha IV hadi VI hayatakubaliwa
- Barua ya maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza
- Barua za maombi ziwasilishwe kabla ya tarehe 20 Mei 2025, saa 3:30 asubuhi
๐ฌ Jinsi ya Kutuma Maombi
Tuma kwa njia ya Posta au Email:
๐ฎ S.L.P 23, Liwale
๐ง [email protected]
To apply for this job email your details to ded@liwaledc.go.tz